Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ajira bado changamoto duniani -ILO

Ajira bado changamoto duniani -ILO

Mkurugenzi Mkuu wa shirika la kazi duniani ILO Guy Ryder amesema kumekuwa na mabadiliko makubwa na ya kasi katika ajira duniani kufuatia kuwepo kwa uhitaji mkubwa wa kazi miongoni mwa watu,teknolojia , kukosekana kwa usawa, umaskini na ukuaji mdogo wa uchumi.

Akiongea wakati wa ufunguzi wa kongamano la kimataifa la 102 la kimataifa kuhusu ajira , linaloendela mjini Geneva Ryder amesema masuala hayo yanasababisha changamoto ya kufikia lengo la ajira bora kwa wote.

(SAUTI YA RIDER)

Swali lililo muhimu na ambalo kila mtu anajiuliza na kwa udharura unaoongezeka na mshangao ni kwamba kazi iko wapi? Na mara kadhaa swali hili huulizwa kuhusiana na hali za vijana

Katika kutafuta ufumbuzi pamoja na mambo mengine Ryder amependekeza kuendelea kwa mchakato wa mageuzi ndani ya ILO ulioanza mwaka jana, na pia shirika hilo kujihusisha zaidi na makampuni ya biashara.

Pia amezungumzia mambo mengine manne ambayo ni kazi za kipato kikubwa, kupunguza umaskini, wanawake kazini na mustakabali wa ajira na kusema ILO ina jukumu kubwa kuhakikisha ni kitovu cha kupiga hatua kwa mustakabali wa sayari dunia na kukomesha umaskini uliokithiri duniani