Rais wa Ufaransa kutunukiwa tuzo inayotambuliwa na UNESCO

5 Juni 2013

Rais wa Ufaransa Francois Hollande leo anatazamiwa kutunukiwa tuzo ya amani ya Félix Houphouët-Boigny wakati wa sherehe maalumu zitazofanyika kwenye makao makuu ya shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na Elimu, Sayansi na Utamaduni UNESCO.

 Tuzo hiyo iliasisiwa mwaka 1989 hutolewa mahasusi kwa watu ama taasisi zilizotoa mchango mkubwa wa upatikanaji wa amani duniani. Miongoni mwa wale waliowahi kutunukiwa tuzo hiyo ni pamoja na Nelson Mandela na Frederik W. De Klerk ambao walifanikisha Afrika Kusin kumaliza kipindi cha ubaguzi wa rangi na kukaribisha enzi mpya.

Mapema mwaka huu serikali ya rais Hollande ilituma vikosi vyake kaskazini mwa Mali kwa ajili ya kukabiliana na waasi waliotibua mustakabali wa eneo