Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Waziri mkuu wa china azungumzia njia za kuboresha uchumi duniani

Waziri mkuu wa china azungumzia njia za kuboresha uchumi duniani

Waziri mkuu nchini China Li Keqiang anasema kuwa sekta za kutoa huduma kote duniani zinaweza zikatoa fursa muhimu kwa ukuaji wa uchumi fursa inayohitajika na nchi zinazoendelea. Akihutubi mkutano wa kimataifa kuhusu huduma bwana Li amesema kuwa mabadiliko yanahitajika kufanywa katika sekta ya utoaji huduma ili kuweza kubuni nafasi zaidi za ajira.

Ameuambia mkutano huo kwamba nchi zilizostawi zinastahili kuongoza katika kufungua masoko na kuzisaodia nchi zinazoendelea pia kubuni masoko yao. Bwana Li aliendelea kuema kuwa uchumi wa dunia una nguzo tatu zikiwemo ustawi wa viwanda, mabadilino ya miji na kuboreka kwa kilimo.