Mkataba wa Biashara ya Silaha waanza kutekelezwa

3 Juni 2013

Mkataba wa biashara ya silaha, ambao ni wa kwanza wa aina yake kujadiliwa na kuamuliwa katika Umoja wa Mataifa, ulipitishwa mnamo tarehe 2 Aprili mwaka huu. Leo Juni 3, nchi nyingi wanachama zimejitokeza kuutia saini, na hivyo kuanza rasmi kutekelezwa kwa mkataba huo.

Akiongea wakati wa hafla hiyo, Bi Angela Kane, ambaye ni Mwakilishi Mkuu wa masuala ya kuondoa silaha katika Umoja wa Mataifa , amesema mkataba huo ni muhimu katika kuleta uwajibikaji na uwazi katika biashara ya kimataifa katika silaha,

Mkataba ni wa ATT unatakiwa uwe unaoleta mabadiliko katika maisha ya mamilioni ya watu wanaoteseka kila siku athari za kusambaza silaha kiholela. Unajumuisha aina nyingi za silaha, zikiwemo silaha ndogondogo, na vyote vinavyoambatana na silaha. Unapinga bayana uuzaji wa silaha unaokiuka vikwazo vya silaha vinavyowekwa na Baraza la Usalama, au zile zinazowezwa kutumika dhidi ya raia, au katika ukiukwaji mkubwa wa sheria ya kimataifa.”

Naye Balozi Peter Woolcott wa Australia, ambaye ndiye rais wa kongamano la mwisho la mkataba wa biashara katika silaha, amesema muhimu zaidi ni utekelezaji

Mkataba huu utasaidia kuzuia silaha kusambzwa kiholela na kinyuma na sheria, kutenda uhalifu na kukiuka haki za binadamu na sheria ya kibinadamu, na utachangia amani na usalama kikanda na kimataifa, na kuchangia maendeleo ya kiuchumi. Tuna mkakati mzuri, lakini muhimu zaidi, ni jinsi mkataba huu utakavyotekelezwa ipasavyo.”