Idadi ya wakimbizi wa Syria walio nchi jirani yavuka Milioni Moja na Laki Sita wiki hii

31 Mei 2013

Mashariki ya Kati yaelezwa kuwa nchini Syria idadi ya wakimbizi waliosajiliwa nchi jirani wiki hii imevuka Milioni Moja na Laki sita na shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR linasema hali ya usalama ni tete na operesheni zake zinakabiliwa na ukata. Joseph Msami na taarifa kamili. (TAARIFA YA JOSEPH MSAMI)

Wiki hii pekee idadi ya wakimbizi wa Syria katika nchi za jirani waliojiandikisha katika shirika la Umoja wa Mataifa la wakimbizi UNHCR imefikia milioni moja na laki sita

UNHCR inaendelea kufanya kazi ndani ya Sryia licha ya kukabiliwa na ugumu katika operesheni zake ikiwamo changamoto ya usalama huku Shirika la Uhamiaji duniani IOM likisema zaidi ya wakimbizi 500 wamevuka mpaka kuingia Jordan na kujiandikisha katika kambii iitwayo Zaatari Dan McNorton ni msemaji wa UNHCR anaeleza hali ilivyo kwa wakimbizi wa Syria.

(SAUTI YA DAN McNORTON)

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter