Matumizi ya roboti huenda ikaikuka sheria ya kimataifa

30 Mei 2013

Mtaalamu mmoja wa haki za binadamu kwenye Umoja wa Mataifa wametaka kusitishwa kwa uundaji na matumizi ya roboti. Wakisema kuwa matumizi ya silahakamahizo hayatakubalika kwa kuwa hazitawajibika kisheria. (TAARIFA YA JASON)

Roboti hizo hufanya kazi pekeyao zikiwa na mitambo ya tarakilishi ambayo huamua ni nani wa kulengwa. Christof Heyns mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu masuala ya kunyongwa kinyume na sheria ametaka kuwa kusitisha matumizu ya robotikama hizo kutatoa nafasi ya kufanyika kwa majadadiliono  kuhusu silaha zinazoua bila ya kuingiliwa na binadamu. Kupitia kwa ripoti kwa baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa bwana Hynes anasema kuwa kuwepo kwa roboti hizo kunaleta wasi wasi mwingi kuhusu usalama wa watu wakati wa vita na pia wakati wa amani. Anasema kuwakama uundaji wake hautangaaliwa kwa makini  basi mitambo ndiyo itakuwa ikiamua ni nani wa kufa na wa kuishi

“Hakuna taifa linalotumia silaha ambazo zinawekwa kwenya orodha ya roboti hizo lakini teknolojia tayari ipo au itakuwepo hivi karibuni. Idadi ya mataifa yaliyo na teknolojia hii yameahidi kutotumia roboti hizo. Hata hivyo ni wazi kuwa mawimbi makali ikiwemo teknolojia na bajeti vinavuta upande mwingine. Roboti hizi pia  zinaweza kutumiwa na serikali dhalimu kuzima wapinzani. Baraza la haki za binadmu linastahili kutoa wito kwa mataifa yote kutangaza na  kutekeleza usitishaji  wa kuundwa , kusafirisha , kutoa na matumizi wa roboti  hadi mpangilio kuhusu roboti hizo utakapobuniwa.”