Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Naibu Mkuu wa WFP akamilisha ziara Syria kwa kutembelea maeneo yenye shida ya chakula

Naibu Mkuu wa WFP akamilisha ziara Syria kwa kutembelea maeneo yenye shida ya chakula

Naibu Mtendaji Mkuu wa Shirika la mpango wa chakula duniani WFP Amir Abdulla leo amekamilisha ziara yake ya siku mbili nchini Syria ambako ametathmini hali ya usambazaji wa misaada ya chakula kwa watu zaidi ya milioni mitatu, katika kipindi cha mwezi Julai mwaka huu. Grace Kaneiya anaripoti

(RIPOTI YA GRACE KANEIYA)

Akiwa nchini humo,Abdulla alitembelea maeneo nje ya Mji wa Damascus na kufanya mazungumzo na raia ambao hupokea msaada wa chakula kutoka WFP .

WFP kila mwezi huwalisha zaidi ya watu 100,000 walioko katika eneo la Al-Kisweh ikiwa sehemu yake utoaji huduma za dharura kwa ajili ya kunusuru maisha ya watu.

Ama afisa huyo alipata fursa ya kukutana maafisa kadhaa wakiwemo Naibu Waziri wa Mambo , waziri wa Ustawi wa Jamii na maafisa wa WFP.