UNAMA yalaani shambulio kwenye ofisi ya chama cha msalaba mwekundu Jalalabad:

30 Mei 2013

Mpango wa Umoja wa Mataifa wa msaada nchini Afghanistan UNAMA umelaani vikali shambulio lililofanyika dhidi ya ofisi ya kamati ya kimataifa ya chama cha msalaba mwekundu ICRC mjini Jalalabadi kwenye jimbo la Mashariki la Nangarh Jumatano ya Mai 29 mwaka huu.Kwa mujibu wa ICRC wafanyakazi wake wawili mmoja wa kimataifa na mwingine wa kitaifa wamejeruhiwa kwenye shambulio hilo huku mlinzi mmoja akiuawa. Wakati wa shambulio hilo baadhi ya wafanyakazi wa kimataifa walihamishwa na kupelekwa kwenye eneo lenye usalama.

UNAMA inasema ICRC inajukumu kubwa na muhimu la kibinadamu nchini Afghanistan na kusisitiza kwamba mashambulio kama hayo dhidi ya wahudumu wa misaada na wauguzi hayaruhusiwi chini ya sheria za kimataifa. Na wafanya kazi hao wanapaswa kuheshimiwa na kulindwa wakati wote.

 

♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter