Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNESCO yalaani mauaji ya mwandishi habari Yemen

UNESCO yalaani mauaji ya mwandishi habari Yemen

Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na elimu, sayansi na utamaduni UNESCO amelaani vikali tukio la kuuliwa kwa mwandishi wa habari wa Yemen Jamal Ahmed Al-Sharabi, aliyeuwawa kwa shambulizi la risasi wakati wa maandamano yanayoendelea mjini Sanaa.

Mtu mmoja aliyekuwa na silaha alishambulia kwa risasi msafara wa waandamanaji kama njia ya kuitaka kudhibiti maandamano hayo, tukio ambalo lilishuhudia pia mamia ya watu wakijeruhiwa. Taarifa zilizotolewa na shirika moja la habari zinasema kuwa mwandishi huyo wa habari aliyeuwawa alikuwa katika moja ya majukumu yake kufuatilia maandamano hayo.

Mkuu wa UNESCO Irina Bokova amesema kuwa kuwawa kwa mwandishi huyo wa habari ni ukandamizaji na uonevu unaodhihiri dhidi ya haki za misingi kwa watu wa Yemen juu ya uhuru wao wa kutoa maoni na kujieleza.