Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Dozi moja tu yatosha kukinga homa ya manjano: WHO

Dozi moja tu yatosha kukinga homa ya manjano: WHO

Shirika la afya duniani WHO linasema sasa dozi moja tuu ya chanjo ya homa ya manjano inatosheleza kumpa mtu kinga ya maisha dhidi ya maradhi hayo.

Masharti ya sasa ya kimataifa yanahitaji mtu anayesafiri au kuishi katika nchi ambazo zinaathirika na homa ya manjano kupata chanjo mbili ya kwanza na ya marudio miaka kumi baadaye. Kwa mujibu wa shirikahilohakukuwa na ushahidi wa kuthibitisha kwamba chanjo ya awali inapungua nguvu yake baada ya muda.

Hata hivyo WHO inasema chanjo bado ni njia muhimu ya kuzuia homa ya manjano na wasafiri bado watawajibika kuonyesha kadi ya chanjo dhidi ya maradhi hayo. Dr Philippe Duclos ni afisa mshauri wa  afya wa WHO.

(SAUTI YA DR PHILIPPE DUCLOS)

(SAUTI YA DR PHILIPPE DUCLOS)

“Tofauti na fikra za zamani ambazo zilidhania kuwa unahitaji dozi ya ziada kuchochea chanjo ya homa ya manjano kila baada ya miaka Kumi, jopo la wataalamu limependekeza kuwa dozi moja tu inatosha kumlinda mtu kwa kipindi cha uhai wake wote na kwamba chanjo ya ziada haihitajiki. Ubora wa chanjo ambayo imekuwa ikitolewa miaka yote haujabadilika na unadumu kipindi chote. Tutashirikiana na nchi wanachama ili kupata njia bora zaidi ya kurekebisha uhalali wa kipindi cha hati ya chanjo.”

Homa ya manjano ni maradhi ynayoambukizwa na mbu, na yaathiri nchi 44 za Afrika na Amerika.