Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Teknohama yakomboa wafanyabiashara wanawake

Teknohama yakomboa wafanyabiashara wanawake

Wakati mkutano wa dunia kuhusu Jamii-Habari ukiendelea hukoGeneva, Uswisi imebainika kuwa maendeleo ya teknolojia ya habari na mawasiliano, teknohama yamekuwa mkombozi kwa wafanyabiashara wanawake ambapo hivi sasa wanaweza kutumia mawasilianokamaya simu au intaneti kutangaza bidhaa zao kwa gharama nafuu. Shirika la Umoja wa Mataifa la Biashara na Maendeleo UNCTAD  na lile la kazi, ILO yanahakikisha kuwa wajasiriamali wanawake wanaimarisha biashara zao kupitia mitandao ya kijamii na hata simu za mkononi. Mmoja wa washiriki wa mkutano huo ni Blandina Sembu kutokaTanzania.

(SAUTI BLANDINA)