Bi. Ogata asisitiza usaidizi kwa wanaoishi kwenye mazingira magumu

9 Mei 2013

Mkutano kuhusu usalama wa binadamu umemealizika hapa mjini New York, ambapo mwenyekiti wa heshima wa bodi inayohusiana na masuala hayo.

Bi. Sadako Ogata amezungumzia umuhimu wa kuwapatia uwezo watu wanoishi katika mazingira magumu akisema kuwa ukosefu wa usalama wa maisha ni moja ya chanzo cha matatizo makubwa duniani. Maelezo zaidi na Alice Kariuki

 (Taarifa ya Alice)

Bi. Ogata amesema uwezeshaji wa watu wanaoisha katika mazingira magumu ili waweze kuchukua hatua za kuhakikisha usalama wa maisha na jamii zao ni suala ambalo limekubalikakama kipaumbele cha juhudi za maendeleo na za kibinadamu.

Amesema ili kuwe na mafanikio katika hali hii Umoja wa Mataifa umeanzisha miradi takriban 200 katika nchi 85 kwa kutumia msaada wa fedha kutoka mfuko wa binadamu kwa ajili ya mpango wa usalama wa binadamu.

 Ameongeza kuwa suala la mpango huu wa usalama wa binadamu limekua chombo muhimu cha kuwezesha watu.

(SAUTI YA OGATA)

"Nadhani tunaweza kusema kuwa mpango wa usalama wa bindamu umekuwa chombo muhimu kwa ajili ya kulinda na kuwezesha watu. Katika kutekeleza mpango huu, jumuiya ya kimataifa imetambua kuwa maisha, riziki na heshima ya watu ndio msingi wa kufikia amani na  maendeleo kwa binadamu."