Mdororo wa kiuchumi waathiri fursa za ajira kwa vijana

8 Mei 2013

Shirika la kazi duniani, ILO leo limetoa ripoti yake inayobainisha kuwa zaidi ya vijana Milioni Sabini na Tatu duniani kote wanatarajiwa kupoteza fursa zao za ajira kwa mwaka huu wa 2013 kutokana na kusuasua kwa uchumi. Jason Nyakundi ana maelezo zaidi.

 (TAARIFA YA JASON)

Ripoti hiyo inasema kuwa  ukuaji wa uchumi kwa mwendo wa kinyonga kwa mwaka mmoja uliopita umechochea kuongezeka kwa tatizo la ukosefu wa ajira kwa vijana . ILO inasema kuwa tatizo la ukosefu wa kazi miongoni mwa  vijana litazidi kushuhghulikiwa kwa miongo kadha inayokuja. Mkurugenzi kuhusu sera kwenye Shirika la kazi duniani ILO Jose Manuel Salazar – Xirinachs anasema jitihada zinahitaji  katika ukuaji wa uchumi na kuboreka kwa elimu na mifumo ya utoaji mafuzno .

(SAUTI YA JOSE)

 “ukuaji ulio wa juu ni muhumu lakini hautoshi . Katika viwango vya kitaifa tunapendekeza hatua zinazolenga ajira kwa vijana. Hii inajumuisha hatua kuhakikisha kuwa vijana wana ujuzi unaohitajika na waajiri na kuwa bishara ndogo na zile na wastani zimepata mikopo ya kuziwezesha kuajiri vijana zaidi. Na kuwa vijana wawe na mazingira ya kufanya kazi sawia na ya watu wazima, na pia wapate mafunzo wakati wanapoendelea na kazi na kusaidia waajiri kuwapa vijana wasiobahatika na kuwandolea ushuri na malipo ya uzeeni kwa kipindi fulani.”

Ripoti hiyo ya ILO inasema kuwa eneo la Mashariki ya kati linazidi kuwa na idadi kubwa zaidi ya vijana wasio na ajira ambapo karibu asilimia 30 ya vijana hawana kazi. Kwa mataifa yaliyostawili vijana wasio kazi ni karibu asilimia 20.