Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tuwaenzi wahanga kwa kutokomeza silaha za kemikali: Ban

Tuwaenzi wahanga kwa kutokomeza silaha za kemikali: Ban

Kutokomeza silaha za kemikali na silaha zingine zote za mauaji wa halaiki ndiyo njia bora ya kuwaenzi wahanga wa silaha hizo na kuvikomboa vizazi vijavyo kutokana na hatari ya silaha hizo. Ujumbe huo umetolewa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, leo Aprili 29, ambayo ni siku ya kimataifa ya kuwakumbuka waathiriwa wa silaha za kemikali.

Bwana Ban amesema maadhimisho ya mwaka huu yana umuhimu mkubwa hata zaidi kwani yanafanyika wakati dunia ikikabiliwa na jinamizi la matumizi ya silaha za kemikali, kutokana na madai ya hivi karibuni kuwa huenda zimetumiwa nchini Syria.

Madai hayo, amesema Katibu Mkuu, ni ukumbusho wa umuhimu wa nchi zote kurithia na kutekeleza Mkataba kuhusu Silaha za Kemikali, kwani kufikia sasa, ni takriban asilimia 80 ya nchi zote zimeurithia mkataba huo.