Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban arejelea wito wa kusimamishwa mapigano Syria

Ban arejelea wito wa kusimamishwa mapigano Syria

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amekutana na mwenzake wa Jumuiya ya nchi za Kiarabu Arab League Nabil Elaraby,ambao kwa pamoja wamejadilia haja ya kupatikana suluhu juu ya mgogoro wa Syria.

Viongozi hao pamoja na mjumbe maalumu kwenye mzozo huo Lakhdar Brahimi wamejadilia haja ya kuzileta pande zote kwenye meza ya majadiliano

Katika mkutano huo uliofanyika kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa New York Ban alirejelea mwito wake wa kulitaka Baraza la Usalama kuchukua hatua za haraka ili kutanzua mzozo huo.

Alisema baraza hilo linapaswa kutafuta njia ya kuwa na Umoja na kuanzisha mchakato wa mjadala wa kisiasa ili kusitisha mapigano na hatimaye kupatikana suluhu ya kudumu.