Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ufadhili wa misitu hauwezi kutegemea chanzo kimoja tuu:Benki ya Dunia

Ufadhili wa misitu hauwezi kutegemea chanzo kimoja tuu:Benki ya Dunia

Ufadhili wa sekta ya misitu lazima utoke katika vyanzo mbalimbali vikiwemo vya ndani na vya kimataifa , pamoja na sekta binafsi. Lakini tatizo la ufadhili wa sekta hiyo haliwezi kufumbuliwa kwa kutegemea chanzo kimoja.

Hayo yamesemwa na Tuuka Castren mtaalamu na afisa wa wa masuala ya misitu, kilimo na maendeleo ya vijijini wa Benki ya dunia katika kitengo cha ufadhjili wa misitu.

Ameongeza kuwa wakati huohuo inatambulika kwamba ili kuchagiza udhibiti endelevu wa masuala ya misitu ufadhili binafsi lazima ubebe jukumu muhimu.

Akizungumza na Radio ya Umoja wa mataifa ametaja baadhi ya changamoto zinazokabili ufadhili kutoka vyanzo binafsi.

(SAUTI YA TUUKA CASTREN)