Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Bidhaa za Maziwa zainua bei za vyakula mwezi Machi:FAO

Bidhaa za Maziwa zainua bei za vyakula mwezi Machi:FAO

Shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na Kilimo, FAO limesema kiwango cha bei za vyakula kwa mwezi uliopita wa Machi kiliongezeka angalau kwa asilimia Moja ikilinganiswa na mwezi uliotangulia wa Februari na kichocheo ni bidhaa zitokanazo na maziwa. Jason Nyakundi anamulikia zaidi habari hiyo.Makadirio ya Shirika la kilimo na mazao la Umoja wa Matataifa FAO kuhusu uzalishaji wa nafaka na mahitaji yake yanaonyesha kurudiwa kwa asilimia fulani ya uzalishaji wa mwaka 2012 ambao umepungua kwa asilimia 2 ikilinganisha na uzalishaji wa mwaka 2011.

Uzalishaji wa nafaka mwaka 2013 kote duniani unatarajiwa kuboreka. FAO inasema kuwa kuna matarajio kwa mazao ya nafaka  kwa ujumla huku mazao ya ngano yakitarajiwa kuwa mazuri pamoja na kilimo cha mchele.

Mazao ya ngano duniani mwaka 2013 yanatarajiwa kuongezeka kwa asilimia 4 hadi tani 690 kikiwa kiwango cha pili cha juu zaidi baada ya kile cha mwaka 2011 cha tani milioni 700.

Hata hivyo bei za maziwa zilipanda kwa pointi tatu  hali ambayo imechangiwa pakubwa na  mabadilko ya hali ya hewa inayochangia kushuka kwa uzalishaji wa maziwa na kupelekea kupungua kwa bidhaa zinazotokana na maziwa.