Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Syria itoe ushirikiano kwa jopo la uchunguzi wa silaha za kemikali: Ban

Syria itoe ushirikiano kwa jopo la uchunguzi wa silaha za kemikali: Ban

Katibu Mkuu wa Umoja  wa Mataifa Ban Ki-Moon amezungumza kwenye mkutano wa nchi wanachama wa mkataba wa kimataifa wa kudhibiti silaha za kemikali huko The Hague, na kurejelea wito wake kwa serikali ya Syria kutoa ushirikiano wa kutosha kwa jopo maalum alilounda kuchunguza madai ya matumizi ya silaha za kemikali nchini humo.

Halikadhalika amesema ni matumaini yake kuwa washiriki wa mkutano huo wataibuka na mbinu za kuwezesha matumizi salama ya kemia kwa manufaa ya kiuchumi.