Hatua ya kutoa huduma ya maji safi zaendelea nchini Kenya

1 Aprili 2013

Wakati malengo ya milenia yakifikia kilele chake mwaka 2015, nchi mbalimbali zina pilika za kukamilisha malengo hayo mojawapo ikiwa ni huduma ya maji.

Kwa mujibu wa kitengo cha uchumi wa maendeleo ya jamii cha umoja wa mataifa UNDESA katika nchi zilizoko kwenye ukanda wa jangwa la Sahara zaidi ya robo ya wakazi wake hutumia zaidi ya nusu saa kwa ajili ya kwenda kuchota maji. Miongoni mwa mataifa katika jangwa hilo ni Kenya nchi ambayo iko mashariki mwa Afrika.

Kenya imepiga hatua  katika  kutoa huduma ya maji safi na salama kwa wananchi wake. Kwa mujibu wa tovuti ya serikali hiyo, huduma ya maji safi inapatikana kwa asilimia 59 huku pia kukiwa na changamoto kadhaa.

Mathalani vijijini bado huduma hiyo haijawafikia watu wengi.Takwimu pia zinaonyesha kwamba ni  makampuni 9 tu  yanaoyotoa huduma endelevu ya maji kati ya makampuni 55 ya maji nchini humo.Ungana na Jasson Nyakundi anayeangazia namna wananchi wa Kenya wanavyopata huduma hiyo ya maji.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter