Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mahojiano na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, na Watoto, ya Tanzania Bi. Mariam Joy Mwaffisi

Mahojiano na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, na Watoto, ya Tanzania Bi. Mariam Joy Mwaffisi

Wajumbe kwenye mkutano wa Kamisheni juu ya Hali ya Wanawake walijadili kwa mapana marefu namna ya kuhamasisha haja ya wanawake na wanaume kufanya kazi pamoja katika majukumu ya malezi, kuwahudumia waathiriwa wa HIV na Ukimwi, pamoja na majukumu ya nyumbani.

Abdushakur Aboud alizungumza na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto ya Tanzania, Bi. Mariam J. Mwaffisi, aliyehudhuria mkutano huo katika Makao Makuu ya UM mjini New York .