Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNHCR inasema asilani wakimbizi wa Kisomali wasirejeshwe nyumbani

UNHCR inasema asilani wakimbizi wa Kisomali wasirejeshwe nyumbani

Maelfu ya wakim,bizi wa Kisomali wanafungasha virako kila siku kutoroka vita nchini mwao.Kwa zaidi ya miongo miwili sasa hali ya usalama nchini Somalia imekuwa tete na kusababisha hofu hata katika nchi jirani za pembe ya Afrika.

Maelfu ya watu hao wanaokimbia vita baina ya serikali na makundi ya wanamgambo wengi huishia nchi za magharibi ambako wengine hupata hifadhi ya wengine kurejeshwa nyumbani.

Sasa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR linasema kuwarejesha nyumbani wakimbizi hao ni kuwatia kitanzi kwani mambo hayajatengamaa hivyo inataka popote wanakokimbia wapewe hifadhi, kwa nini? Yusuf Hassan msemaji wa UNHCR anafafanua