Ban asifu MONUSCO kupatiwa mamlaka mpya

28 Machi 2013

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon ameunga mkono hatua aliyoitaja kuwa ni muhimu ya Baraza la Usalama kupitisha azimio juu ya Jamhuri ya Demokrasi ya Kongo, DRC ambalo linaipatia ujumbe wa Umoja huo nchini humo MONUSCO mamlaka mpya.

Katika taarifa yake Ban amesema azimio hilo ni hatua madhubuti ya kushughulikia chanzo cha mgogoro Mashariki mwa DRC na Ukanda mzima wa Maziwa Makuu.

Amesema ana imani kuwa azimio hlo litawezesha Umoja wa Mataifa kusaidia utekelezaji wa mpango wa amani, utulivu na ushirikiano uliotiwa saini mwezi Februari mwaka huu huko Addis Ababa na kwamba mjumbe wake maalum kwa nchi za Maziwa Makuu Mary Robinson atashiriana vyema na wadau wote kusongesha mbele mchakato.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud