Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wananchi wa Somalia waanza kufurahia matunda ya amani

Wananchi wa Somalia waanza kufurahia matunda ya amani

Mwanzoni mwa wiki hii mjini Mogadishu kulifanyika shambulizi la bomu lililosababisha vifo vya watu saba na wengine kadhaa kujeruhiwa. Mwakilishi maalum wa katibu mkuu wa umoja wa mataifa nchini Somalia Balozi Augustine Mahiga,  alilaani shambulizi hilo linalosemekana lilimlenga Afisa wa usalama, na kusema hilo litaongeza ari ya wasomali katika kusaka amani.

Wakati hayo yakiripotiwa utafiti wa kikosi cha Muungano wa Afrika nchini Somalia AMISOM, unaonyesha utulivu umeimarika nchini humo tangu mwaka 2011. Hali ikoje kwa sasa? Ungana na Joseph Msami katika taarifa hii.