Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mchakato wa kura ya maoni Sudan umeenda shwari asema mwangalizi wa UM:Mkapa

Mchakato wa kura ya maoni Sudan umeenda shwari asema mwangalizi wa UM:Mkapa

Wasudan Kusini wapatao milioni 4 kuanzia Jumapili iliyopita Januari 9 wanapiga kura kuamua hatma yao, je Sudan Kusini ijitenge na Kaskazini na kuwa taiofa huru ala la.

Uamuzi wa kufanyika kura hiyo umo kwenye makubaliano ya amani ya 2005 yajulikanayo kama CPA. Kwa mujibu wa jopo la Umoja wa Mataifa la kuangalia kura hiyo hadi sasa mambo yamekwenda salama salimin, bila purukushani yoyote kubwa ya kutia dosari. Upigaji kura unakamilika Jumamosi hii Januari 15 na kitakachosubiriwa ni kutangazwa kwa matokeo.

Kama Wasudan kusini wataamua kujitenga basi wataandika historia ya kuwa taifa la 54 barani Afrika. Flora Nducha amezungumza na mwenyekiti wa jopo la Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa la kuangalia kura hiyo Rais mstaafu wa Tanzania Benjamin Mkapa akiwa mjini Khartoum kuhusu mchakato mzima wa kura hiyo

(MAHOJIANO NA MKAPA)