Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

FAO yahamasisha Uganda iendeleze kilimo cha biashara

FAO yahamasisha Uganda iendeleze kilimo cha biashara

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Kilimo na Chakula duniani, FAO José Graziano da Silva amesifu serikali ya Uganda kwa uongozi wake thabiti wa kuimarisha sekta ya kilimo na kupunguza madhara ya mabadiliko ya tabia nchi.

Da Silva Ametoa pongezi hizi wakati wa ziara yake ya siku moja nchini humo ambapo alikuwa na mazungumzo na Makamu wa Rais Edward Sekandi. Wawili hao wamejadili mbinu za kuhakikisha usalama wa chakula kwa wote nchini Uganda na kupunguza umaskini kwa kuunga mkono juhudi za wakulima wadogo. Jason Nyakundi na maelezo zaidi.

(SAUTI JASON)