Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uvunaji wa zao la ngano watazimiwa kuongezeka mwaka 2013

Uvunaji wa zao la ngano watazimiwa kuongezeka mwaka 2013

Uvunaji wa zao la ngano katika kipindi cha mwaka 2013,inatazamiwa kuongezeka na kufikia tani milioni 690 ikiwa ni ongezeko la asilimia 4.3 ikilinganishwa na mwaka uliopita huku mapigano katika baadhi ya nchi yakiripotiwa kukwamisha uhakika wa chakula.   Takwimu zilizotolewa na shirika la chakula na kilimo duniani FAO zinaonyesha kiwango cha mavuno kinatazamiwa kuongezeka zaidi katika nchi za Ulaya.  Urusi ndiyo iliyotajwa kuongeza msukumo zaidi kwenye kilimo cha ngano kupitia mpango wake wa kukabiliana na tatizo la ukosefu wa chakula kwa bara la Ulaya kwa kuanzisha mpango maalumu ambao unatoa msukumo uendelezaji zao hilo. George Njogopa na maelezo zaidi.