Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watoto wa kipalestina huko Israel wahakikishiwe usalama: UNICEF

Watoto wa kipalestina huko Israel wahakikishiwe usalama: UNICEF

Shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa limetoa mpangilio wa hatua ambazo zitachukuliwa ili kuboresha hali ya watoto wa kipalestina wanaozuiliwa na jeshi la Israel. Kupitia kwa taarifa yenye kichwa “watoto walio kwenye kizuizi cha jeshi la Israel” UNICEF inapendekeza kutendewa  vyema watoto kipalestina walio kwenye kuzuizi cha jeshi la Isael kuambatana na viwango vya kimataifa vya haki za watoto na vile vingine vya kimataiafa. Ripoti hiyo iliyotolewa kuambatana na ushuhuda unaohusu haki za watoto walio kizuizini inadai kuwa watoto hao wamekuwa wakitendewa vibaya wanapohojiwa au wanapoahamishwa. Jason Nyakundi na taarifa zaidi.

(SAUTI YA JASON)