Mtaalamu wa UM ataka kuwekeza kwa wanawake kukabili njaa

4 Machi 2013

Mtaalamu huru wa Umoja wa Mataifa amesema kuwa kumwezesha mwanamke kwa hali yoyote ni sawa na kuchukua njia ya mkata ya kukabiliana na tatizo la ukosefu wa chakula, tatizo ambalo limeendelea kuwa sugu katika maeneo mengi.

 

Olivier De Schutter ambaye ni mtaalamu juu ya haki ya chakula amesema kuwa viongozi wa dunia wanapaswa kuzifanyia marekebisho sera zao ikiwemo pia kukaribisha mageuzi kwenye maeneo ya utamaduni ili kuondoka na fikra kandamizi dhidi ya wanawake.

 

Mtaalamu huyo amekaribisha sera zinazopigania usawa na kumkomboa mwanamke akisema kuwa mipango ya mageuzi inayoendelea kushuhudiwa sasa nchini India ni ishara njema ya kukabiliana na tatizo la ukosefu wa chakula.

Ametaka dunia kutambua kuwa, inayo fursa ya kushinda tatizo la njaa kwa kuendelea kuwekeza kwa wanake ambao amewaelezea kuwa ni nguzo muhimu katika ujenzi wa familia.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter