Skip to main content

Mkutano wa Shirika la Uhamiaji (IOM) wakamilika nchini Tanzania

Mkutano wa Shirika la Uhamiaji (IOM) wakamilika nchini Tanzania

Shirika la Kimataifa linalohusika na uhamiaji IOM, limehitimisha mkutano wake wa siku tatu nchini Tanzania uliowajumuisha maofisa wa uhamiaji kutoka baadhi ya nchi wanachama wa jumuiya ya maendeleo kusini mwa Afrika SADC, na kuanisha vipaumbele vinavyopaswa kuzingatiwa ili kukabiliana na wimbi la wahamiaji haramu.

George Njogopa na taarifa zaidi.

Maafisa hao uhamiaji wamejadilia haja ya kuimarisha taaluma ya utambuzi katika maeneo ya mipakani pamoja na uwekaji udhibiti kwenye hati za kusafiria.

Mkutano huo umefanyika katika wakati ambapo Tanzania ikiendelea na juhudi za kuwasajili raia wake kwa ajili ya kuwapatia vitambulisho, hatua ambayo inatajwa kuwa huenda ikasaidia kupunguza tatizo la wahamiaji haramu.

Afisa wa shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na uhamiaji, Marcellino Ramkishani pamoja na kupongeza hatua ya uanzishwaji wa vitambulisho vya taifa, lakini pia amejadilia haja ya nchi wanachama kwenye eneo hilo kuwa na mifumo inayoweza kuwasiliana kirahisi.

Kwa upande mwingine amesema kuwa ‘ Mkutano huu wa usimamizi wa vitambulisho umetoa fursa kwa washiriki kupata ujuzi zaidi ya yote ni kuwa na taarifa kwa serikali namna wanavyoweza kujilinda.

Akizungumza baada ya mkutano huo, Kamishna wa uhamiaji nchini Tanzania Abbas Irovya alisema kuwa

Mkutano huu ulihudhuria na maofisa uhamiaji toka nchi za Msumbiji, Malawi, Zambia na wenyeji Tanzania.