Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wakulima Ethiopia wanufaika na mpango wa P4P: WFP

Wakulima Ethiopia wanufaika na mpango wa P4P: WFP

Shirika la mpango wa chakula la Umoja wa Mataifa, WFP limetangaza mafanikio makubwa ya mpango wake wa ununuzi wa chakula kwa maendeleo, P4P nchini Ethiopia baada ya vyama vya ushirika kuliuzia shirika hilo kiasi kikubwa cha chakula kinachotosha kulisha watu Milioni Moja nukta nane nchini humo kwa mwezi mzima.  Taarifa zaidi na Assumpta Massoi.

(Sauti ya Assumpta)

Mpango huo unatokana na makubaliano yaliyotiwa saini kabla ya msimu wa kilimo uliopita kati ya shirika hilo na vyama 16 vya ushirika ambapo wakulima wananufaika kwa kuuza mazao yao karibu, huku WFP ikiwa haitumii gharama kubwa kusafirisha chakula cha msaada kwa waethiopia wenye njaa pamoja na wakimbizi.  Mwakilishi mkazi wa WFP nchini Ethiopia, Abdou Dieng amesema lengo la mpango huo ni kuhakikisha Ethiopia inajilisha yenyewe  na inakuwa ni gharama nafuu kwa kuwa pia wanakuwa wanasaidia wakulima wadogo kuwa na masoko karibu.  WFP pia inawapatia wakulima msaada wa kiufundi ikiwemo vifaa, jinsi ya kuhifadhi mazao baada ya mavuno na usafirishaji ili kuhakikisha vyama vya ushirika vinatimiza mkataba wa kuwasilisha kiasi cha mazao kinachohitajika.