Bara la Afrika laungana kudhibiti majanga ya asili

13 Februari 2013

Wawakilishi kutoka nchi 40 za Afrika wanakutana huko Arusha, Tanzania kujadili njia za kuzuia na kupunguza athari za za majanga wakati huu ambapo ulimwengu unaoendea kuathiriwa na mabadiliko ya tabianchi, ukame, mafuriko , kupanda kwa joto, moto wa misistuni na majanga mengine ya kiasili.

Kulingana na makadirio kutoka kituo cha utafiti wa hali ya hewa na Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na kupunguza athari za majanga, UNSDR, ni kwamba watu milioni 18 waliathiriwa na ukame mwaka uliopita huku milioni 8.8 wakiathiriwa na mafuriko katika eneo la kusini mwa jangwa la sahara. Hasara iliyopatikana kutokana na majanga hayo kwa muda wa miaka miwili ilikuwa ni gharama ya dola bilioni 1.3. Jason Nyakundi na taarifa kamili.