Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM wapongeza bunge la Ufilipino kwa kupitisha muswada wa kulinda wakimbizi wa ndani

UM wapongeza bunge la Ufilipino kwa kupitisha muswada wa kulinda wakimbizi wa ndani

Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR limepongeza hatua ya bunge la Ufilipino la kupitisha muswada wa sheria wa kulinda haki za wakimbizi wa ndani nchini humo.

Muswada huo uliopitishwa wiki hii utakuwa sheria pindi utakapotiwa saini na Rais Benigno Aquino wa III, na hivyo kuifanya Ufilipino kuw anchi ya kwanza kwenye ukanda wa Asia na Pasikifi kuwa na sheria ya kina ya kulinda utu na haki ya wakimbizi wa ndani kwa mujibu wa viwango vya kimataifa hususan mwongozo wa Umoja wa Mataifa wa kulinda wakimbizi wa ndani.

Mwakilishi wa UNHCR nchini Ufilipino Bernard Kerblat amesema hatua hiyo ni muhimu kwa Ufilipino ambayo kwa miongo kadhaa imegubikwa na mizozo ikitaja maeneo ya Mindanao ambapo hadi sasa kuna wakimbizi wa ndani Laki Tatu. Amesema ni matumaini yake nchi zingine kwenye ukanda huo zitaiga mfano na kupitisha sheria za aina hiyo.

Muswada huo unataja haki za wakimbizi wa ndani wakati wa mizozo na adhabu kali dhidi ya yeyote atakayesababisha ukimbizi wa ndani holela ikiwemo watu wasio wapiganaji ambao wanakumbwa katikati ya mizozo