Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Rushwa yagharimu Afghanistan dola Bilioni 3.9: UM

Rushwa yagharimu Afghanistan dola Bilioni 3.9: UM

Afghanistan imetajwa kupiga hatua juu ya kukabiliana na vitendo vya rushwa katika ofisi za umma, lakini hata hivyo mafanikio hayo bado ni ya kiwango cha chini.

Uchunguzi uliofanywa na Mashirika ya Umoja wa Mataifa umebaini kuwa pamoja na kuwepo kwa idadi  ndogo ya watu wanajihusisha na vitendo vya rushwa, lakini fedha zilizotokana na mwenendo huo zilifikia dola za Marekani bilioni 3.9 na hii ikiwa ni ongezeko la asilimia 40 katika kipindi cha kuanzia mwaka 2009 hadi 2012.

Ripoti ya pamoja iliyotowa na Ofisi ya Umoja wa Mataifa unayohusika na usimamizi wa vitendo vya rushwa na ile ya kukabiliana na madawa ya kulevya na vitendo vya uhalifu UNODC, imesema kuwa nusu ya karibu ya nusu ya wakanchi wa Afghanistan walilazimika kutoa rushwa ili kupata huduma kwenye ofisi za umma Taarifa zaidi na George Njogopa.

(SAUTI YA GEORGE)