Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Teknolojia ya mawasiliano yaimarisha huduma za posta: UPU

Teknolojia ya mawasiliano yaimarisha huduma za posta: UPU

Mkurugenzi Mkuu mpya wa Muungano wa mashirika ya posta duniani, UPU Bishar Hussein amesema kadri teknolojia ya mawasiliano inavyoimarika ndivyo ilivyo kwa huduma za posta na hivyo changamoto ni kwa mashirika ya posta duniani kuwa na ubunifu zaidi ili yaweze kwenda na wakati.

Bwana Hussein ameiambia Radio ya Umoja wa Mataifa katika mahojiano maalum kuwa licha kupungua kwa usafirishaji wa barua binafsi lakini maendeleo ya teknolojia ya mawasiliano yameibua biashara mtandao ambayo imeongeza usafirishaji wa vifurushi vya biashara kwa njia ya posta.

(SAUTI BISHAR)- Hussein UPU Clip

Halikadhalika Bwana Hussein amesema changamoto kubwa inayomkabili ni kuhakikisha mashirika ya posta yanafikia katika kiwango sawa ili yaweze kuzungumza lugha moja na kuboresha huduma kwa maendeleo endelevu.