Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ripoti mpya ya WHO yaonyesha uhaba wa huduma za afya Syria

Ripoti mpya ya WHO yaonyesha uhaba wa huduma za afya Syria

Sita kati ya kila hospitali kumi na tatu, ikiwemo hospitali kuu ya umma katika jimbo la Homs nchini Syria, hazina huduma za matibabu. Hii ni kwa mujibu wa ripoti mpya ya hali ya afya katika muktadha wa mzozo nchini humo, ambayo imetolewa na Shirika la Afya Duniani, WHO.

Ili kuwezesha huduma za afya, shirika la WHO limeweka timu ya huduma za dharura katika eneo la Amman ili kutoa msaada wa kitaaluma na operesheni za ofisi zake nchini Syria na katika nchi jirani za Jordan, Lebanon, Iraq, Misri na Uturuki.

Shirika hilo pia limeweka saini mikataba ya ushirikiano na mashirika yasiyo ya kiserikali katika majimbo ya Idleb, Homs na vitongoji vya mji mkuu Damascus, ili kuwezesha utoaji wa huduma za afya kwa kipindi cha miezi mitatu.

Aidha, raia laki mbili wa Lebanon waliorejea kutoka Syria wanahitaji misaada ya dharura ya kibinadamu na makazi, kwa mujibu wa wizara ya masuala ya kijamii nchini Lebanon. Jason Nyakundi na maelezo zaidi.

(SAUTI YA JASON NYAKUNDI)