Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kumbukumbu za tetemeko la Haiti bado dhahiri

Kumbukumbu za tetemeko la Haiti bado dhahiri

Leo ni miaka mitatu tangu kutokea kwa tetemeko kubwa la ardhi huko

Haiti lililosababisha vifo vya watu zaidi ya Laki Tatu na Mamilioni kupoteza makazi ambapo Umoja wa Mataifa umesema kazi ya ujenzi inaendelea vizuri na asilimia 80 ya taka zitokanazo na tetemeko hilo zimeshaondolewa.

Miongoni mwa walionusurika katika tetemeko hilo ni Jean BERNARDINI, ambaye kwa sasa anafanya kazi na ofisi za UNDP mjini NewYork, Marekani na anasema tetemeko hilo lilichukua sekunde 50 tu hivi lakini mambo mengi yalitokea.

“Mambo mengi yalitokea katika sekunde hizo 50. Mji tulioufahamu haukuwepo tena. Asilimia 80 ya majengo ya serikali yalikuwa chini. Mji ulikuwa umeharibiwa kabisa. Vifusi vya majengo yaliyobomoka kilikuwa na ukubwa wa wa mita Milioni Kumi za mraba. Jengo la Umoja wa Mataifa lilikuwa limebomoka kabisa. Nilihisi kuchanganyikiwa, na nilipata fikrsa kuwa kuna kitu kitaendelea kutokea kama tsunami na pili nilikuwa na mkanganyiko, nawaza sasa na uharibifu huu Haiti inaweza kusimama tena. Kwa kuwa niliona miili ya watu imetapakaa na kulikuwa na uharibifu mkubwa.”

Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, jitihada za kusadia Haiti kurejea katika hali yake ya kawaida zimetia matumaini ikiwemo ujenzi wa shule, upatikanaji wa ajira lakini bado kazi kubwa inahitajika kufanyika.