Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nitaimarisha mtandao wa posta duniani: Hussein

Nitaimarisha mtandao wa posta duniani: Hussein

Mkurugenzi Mkuu mpya wa Umoja wa mashirika ya posta duniani, UPU, Bishar Hussein kutoka Kenya amesema azma yake kubwa ni kuimarisha mtandao wa mashirika ya posta duniani.

Akizungumza mjini Berne, Usiwsi leo wakati wa hafla ya kukabidhiwa ofisi, ili kuchukua wadhifa huo kwa kipindi cha miaka minne, Bwana Hussein amesema atahakikisha nchi zote kuanzia zilizoendelea, zinazoendelea hadi zile za visiwa vidogo zinaunganishwa katika jumuiya ya kimtandao ya mashirika ya posta duniani na kwamba ni lazima kushughulikia mahitaji yote ya wanachama wa UPU kwa pamoja.

Bwana Hussein amewahi kuwa Mtendaji mkuu wa shirika la posta la Kenya na amechukua nafasi hiyo baada ya mkurungenzi mkuu wa zamani Edouard Dayan kumaliza muda wake.