Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Brahimi apendekeza serikali ya mpito nchini Syria

Brahimi apendekeza serikali ya mpito nchini Syria

Msuluhishi wa Umoja wa Mataifa na Jumuiya ya kiarabu kwa mzozo wa Syria Lakhdar Brahimi amependekeza serikali mpito nchini humo itayokuwa kwenye hatamu za uongozi hadi wakati kipindi cha utawala wa rais Bashar Al Assad kitapomalizika mwaka 2014.

Kauli hiyo ambayo imenukuliwa na vyombo vya habari, inafuatia majadiliano ya kina yaliyofanywa baina ya Brahim na rais Assad, majadiliano ambayo pia yaliwajumuisha viongozi mashuhuri wanaopinga utawala wa sasa. Bwana Brahimi ameripotiwa akisema wananchi wa Syria wanataka mabadiliko ya dhati na kwamba mwingilio wa kijeshi nchini Syria siyo suluhu la mzozo huo. George Njogopa na taarifa zaidi.

(SAUTI YA GEORGE NJOGOPA)