Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Teknolojia ya anga za juu kutumiwa kupunguza athari za majanga: ESCAP

Teknolojia ya anga za juu kutumiwa kupunguza athari za majanga: ESCAP

Nchi za Asia – Pasific zimeridhia mpango wa utekelezaji unaotumia teknolojia ya anga za juu kushughulikia majanga ya kiasili na hatimaye kufikia malengo ya maendeleo endelevu kwenye ukanda huo.

Makubaliano hayo yamefikiwa mwishoni mwa mkutano wa siku mbili ambapo mpango huo unataka tume ya Uchumi na kijamii ya Umoja wa Mataifa kwa nchi za Asia na Pasifiki, ESCAP kuhuisha mipango iliyopo ya kikanda na kuweka pamoja utaalamu na rasilimali ili kuimarisha jitihada za kuondoa tofauti zilizopo baina ya nchi za kupunguza madhara ya majanga na hatimaye kuleta maendeleo endelevu.

Akizungumza katika mkutano huo, Msaidizi wa katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ambaye pia ni Katibu Mtendaji wa ESCAP dkt. Noeleen Heyzer amesema teknolojia ya anga za juu bado haijawa na manufaa ya kutosha kwa mtu wa kawaida kwa hiyo changamoto ni jinsi ya kuitumia ili iwe na manufaa.

(SAUTI Dkt. Noeleen Heyzer)