Ubaguzi dhidi ya wapenzi wa jinsia moja au waliobadili jinsi ukome: Yvone Chaka Chaka

11 Disemba 2012

Balozi mwema wa Umoja wa Mataifa  Yvonne Chaka Chaka  ambaye yuko mjini New York Marekani kushiriki tukio la ngazi ya juu la nafasi ya uongozi katika vita dhidi ya ubaguzi dhidi ya wapenzi wa jinsi moja au waliobadili jinsi zao amesema ni wakati muafaka serikali zinazobagua au kuhukumu watu hao zitajwe na ziabishwe kwa kuwa kitendo hicho ni kinyume na haki za binadamu.

Akizungumza na waandishi wa habari, Yvonne ambaye pia ni mwanamuziki mashuhuri wa Afrika Kusini  amesema yeye mwenyewe ana watoto wanne wa kiume na hatojali ni marafiki wa aina au jinsi gani ambao watoto wao watapenda kuishi nao, hivyo Umoja wa Mataifa uchukue nafasi yake.

(SAUTI YA YVONNE)

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter