Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kupima viwango vya risasi mchangani kutapunguza madhara kwa watoto

Kupima viwango vya risasi mchangani kutapunguza madhara kwa watoto

Nchi nyingi, hususani zile zenye historia ndefu ya uchimbaji migodi zinaweza kupunguza kwa kiasi kikubwa madhara ya madini ya risasi miongoni mwa watoto kwa kupima viwango vya uchafuzi wa madini hayo mchangani, ili kutambua ni maeneo yepi yenye hatari, na hivyo kuwaepusha watoto na maeneo hayo. Hayo ni kwa mujibu wa ripoti ya utafiti ilochapishwa katika jarida la Disemba la Shirika la Afya Duniani, WHO.

Utafiti huo ulilinganisha viwango vya uchafu wa risasi mchangani ndani na karibu na maeneo mawili ya uchimbaji migodi nchini Peru, ambayo ni mojawapo ya wazalishaji wakubwa zaidi wa fedha, shaba, dhahabu na zinki. Viwango vya hatari vya madini ya risasi vilipatikana katika mchanga wa Cerro de Pasco, mji wa kihistoria wa uchimbaji migodi, ambako uchimbaji wa shaba bado unaendelea. Taarifa kamili na  Joshua Mmali.

(SAUTI YA JOSHUA MMALI)