Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kiongozi wa mashauriano ya Afrika huko Doha ataka wajumbe wa Afrika kuelewa hoja kwa kina

Kiongozi wa mashauriano ya Afrika huko Doha ataka wajumbe wa Afrika kuelewa hoja kwa kina

Mwenyekiti wa waendesha mazungumzo wa kundi la Afrika Mr. Dlamini Emmanauel ameelezea matumaini kutokana na matokeo ya mkutano kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa yanayoendelea mjini Doha Qatar lakini akasisitiza kuwa kuhudhuriwa kwa vikao na wajumbe kutoka Afrika litakuwa jambo muhimu.

Kwenye mkutano wa kwanza na mtaribu wa kituo cha sera kuhusu hali ya hewa barani Afrika Dr Fatima Denton Bwana Emmanuel amesema kuwa kile ambacho Afrika italeta nyumbani kutoka Doha itategemea na waendesha mazungumzo. Jason Nyakundi na taarifa kamili.

(SAUTI YA JASON NYAKUNDI)