Skip to main content

Mkutano wa utunzaji misitu kufanyika Brazzaville:UM

Mkutano wa utunzaji misitu kufanyika Brazzaville:UM

Maafisa kutoka zaidi ya nchi 35 zilizo kwenye maeneo yaliyo na misitu mikubwa zaidi duniani wanatarajiwa kukusanyika kwenye mkutano unaoungwa mkono na Umoja wa Mataifa mwezi ujao kujadili changamoto zinazoyakumba maeneo hayo yaliyo tegemeo kwa zaidi ya watu bilioni moja.

Mkutano huo wa siku nne ambao utaandaliwa kuanzia tarehe 31 mwezi Mei kwenye mkuu wa Congo Brazzaville pia ni sehemu ya sherehe za kuadhimisha siku ya kimataifa ya misitu mwaka huu.

Kati ya maeneo hayo ni bonde la Amazon lililo Amerika Kusini, Bonde la Congo lilili katika kanda ya Afrika ya kati na bonde la Borneo-Mekong lililo kusini mashariki mwa Asia. Misitu katika maeneo hayo inazidi kutoweka kwa haraka huku uharibifu wa misitu ukichangia asilimia 20 ya gesi chafu inayoingia hewani.