Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Irina Bokova ataka mashirikiano kwenye utamaduni

Irina Bokova ataka mashirikiano kwenye utamaduni

Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na elimu, sayansi, na utamaduni UNESCO Bi Irina Bokova amesema kuwa jamii inapaswa kujengewa mustakabala bora ikiwemo pia kujengewa daraja litalounganisha utamaduni wa watu wote.

Bi Bokova ambaye alikuwa akizungumza kwenye ufunguzi tamasha moja la kimataifa lililofanyika Uturuki, amesisitiza ulazima wa kuunganisha utamaduni wa mataifa .

Tamasha hilo linalopigia upatu mwingiliano wa kitamaduni kwa ajili ya kuimarisha masikizano ya kijamii lilianzishwa kwa mara ya kwanza mwaka 2011na linatajwa kupata mafanikio makubwa.

Mwaka huu tamasha hilo liliratibiwa kwa ushirikiano wa pamoja baina ya UNESCO na serikali ya Uturiki na liliweka zingatio la kukaribisha masikizano.