Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mwaka wa UM wa kuleta pamoja tamaduni wakamilika

Mwaka wa UM wa kuleta pamoja tamaduni wakamilika

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki moon amesema kuwa kushikilia zaidi tamaduni na kutokuwepo uvumilivu huenda kukaongeza mwanya uliopo kati ya tamaduni mbali mbali duniani.

Akiongea wakati wa kukamilika kwa mwaka wa Umoja wa Mataifa wa kuleta pamoja tamaduni tofauti duniani kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa Ban amesema kuwa ana uhakika kuwa uhusiano uliojenga wa kuleta pamoja tamaduni utatekelezwa kwenye miaka inayokuja.

Akiongea kwenye sherehe za kumalizika kwa mwaka huo naye mkurugenzi wa shirika la elimu, sayansi na utamaduni la Umoja wa Mataifa UNESCO Irina Bokova kwa upande wake amesema kuwa ni lazima kuwe na jitihada za kumaliza kutengana kwa jamii na kubuni njia za kuleta pamoja tamaduni zote.