Hatua zichukuliwe kudhibiti mabadiliko ya tabianchi: Benki ya dunia

20 Novemba 2012

Ripoti mpya kuhusu mabadiliko ya tabianchi inadokeza kuwa muda unatokomea kuweza kupunguza madhara yatokanayo na mabadiliko ya tabianchi.

“ Turn down the Heat” au punguza kiwango cha joto, ni jina la ripoti hiyo iliyoandaliwa na taasisi ya mabadiliko ya tabianchi ya Potsdam kwa ajili ya Benki ya Dunia na inaeleza kuwa kiwango cha juu cha joto kinaelekea kuongezeka kwa zaidi ya nyuzi joto Nne ifikapo mwishoni mwa karne hii iwapo jitihada za kudhibiti mabadiliko hayo hazitafanikiwa.

Inaonya kuwa ongezeko hilo litakuwa na ishara mbali mbali ikiwemo mikondojoto mikali kupita kiasi, kupungua kwa akiba ya chakula, kupotea kwa bayonuai na kuongezeka kwa kiwango cha maji ya bahari.

Jim Yong Kim ni Rais wa Benki ya dunia.

(SAUTI YA JIM)

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter