Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Idadi ya vifo na wagonjwa kutokana na homa ya Manjano Darfur yaongezeka: WHO

Idadi ya vifo na wagonjwa kutokana na homa ya Manjano Darfur yaongezeka: WHO

Idadi ya vifo vitokanavyo na homa ya manjano huko Darfur, Sudan imeongezeka na kufikia 110 huku idadi ya wagonjwa nayo pia ikiongezeka na kufikia 374.

Takwimu hizo ni kwa mujibu wa shirika la afya duniani, WHO ambalo katika ripoti yake kuhusu hali halisi ya ugonjwa huo hadi juzi inaonyesha kuwa ugonjwa huo umeenea katika vitongoji vya Darfur ya Kati, mashariki, magharibi na Kusini huku takribani asilimia 70 ya wagonjwa wote wakipatikana Darfur ya Kati.

Idadi kubwa ya wagonjwa hao ni watu wenye umri wa kati ya miaka 15 na 30 ambao ni asilimia 47 nukta tatu ya wagonjwa wote wakifuatiwa na wenye umri wa kati ya miaka 30 na 45 ambao ni asilimia 14 nukta Saba. Taarifa kamili na Monica Morara.

(SAUTI YA MONICA MORARA)