Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mashirika ya UM na wataalam wajadili suluhisho la lishe bora kwa watoto

Mashirika ya UM na wataalam wajadili suluhisho la lishe bora kwa watoto

Mkutano wa aina yake uliofanyika wiki hii kwenye mji mkuu wa Ethiopia Addis Ababa umeimarisha jitihada za kuendeleza hatua za lishe bora kwa watoto kwa mujibu wa mkakati wa kuondoa njaa kwa watoto uitwao REACH.

Wataalamu na maafisa wa mashirika ya Umoja wa Mataifa kutoka nchi 12 zinazotekeleza mpango huo wa REACH, pamoja na Ethiopia walishiriki mkutano huo.

Utekelezaji wa REACH unahusisha msaada wa pamoja unaoratibiwa na Umoja wa Mataifa wa kusaidia serikali kupanua na kujumuisha mikakati mbali mbali ya kimataifa katika vita dhidi ya utapiamlo.