Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mauaji ya wakimbizi wa kipalestina Syria yakomeshwe: UNRWA

Mauaji ya wakimbizi wa kipalestina Syria yakomeshwe: UNRWA

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu misaada kwa ajili ya wakimbizi wa kipalestina, UNRWA limeendelea kuonyesha wasiwasi wake juu ya madhara ya mgogoro wa Syria kwa wakimbizi wa kipalestina na raia wa nchi zingine na hivyo kutaka pande zote katika mgogoro huo kujizuia kufanya mashambulizi ya kiholela kwa mujibu wa sheria za kimataifa.

Wito huu wa UNRWA unafuatia ripoti za hivi karibuni ya kwamba wakimbizi wa kipalestina walikuwa miongoni mwa watu waliouawa kwenye mashambulio yaliyotokea kwenye maeneo tofauti nchini Syria ikiwemo lile la kwenye viunga vya mji mkuu wa Syria, Damascus. George Njogopa na taarifa zaidi.

(SAUTI YA GEORGE NJOGOPA)