Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wiki ya bara la Afrika ndani ya Baraza Kuu la UM

Wiki ya bara la Afrika ndani ya Baraza Kuu la UM

Kila mwaka Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa huwa na juma moja la bara la Afrika. Katika kipindi hicho hufanyika mjadala wa pamoja wa wazi kuhusiana maendeleo ya Afrika, bara lenye idadi kubwa ya wanachama katika chombo hicho cha dunia chenye wanachama 193.

Mwaka huu masuala yaliyomulikwa ni ripoti ya maendeleo ya ushirikiano kati ya Umoja wa Mataifa na nchi za Afrika kupitia ushirikiano mpya wa maendeleo ya Afrika NEPAD, sababu za migogoro barani Afrika na muongo mmoja wa programu ya kimataifa ya kutokomeza malaria iliyoanza kutekelezwa mwaka 2011 katika nchi zilizoendelea ikiwemo zile za barani Afrika. Katika makala haya Assumpta Massoi anamulika juma hilo la Afrika.

(PKG YA ASSUMPTA MASSOI)